Kwa mujibu wa Ripoti Rapa Lil Durk ambae kwa sasa yupo Kizuizini huko Miami kutokana na Mashtaka ya Kukodi watu kwa ajili ya kuua, Amepanga kupinga Mashtaka dhidi yake licha ya tarehe rasmi ya kusikilizwa kesi yake kutokuwekwa wazi.
Kwa sasa inasemekana Lil Durk anatajwa kuwa ni mtu mwenye roho nzuri kwa wafungwa japo kuwa sio mpenzi wa chakula cha rumande.
Wiki iliyopita watu watano ambao walidai kuwa na uhusiano na kundi la rap la Lil Durk la Only The Family na walikuwa washiriki wenza katika njama ya mauaji ya kuajiriwa ya 2022, walikamatwa huko Chicago na kufikishwa katika Mahakama ya Dirksen ya Marekani, Chicago Tribune.