Msanii wa muziki wa AI, Xania Monet, ameteka vichwa vya habari baada ya kupata mkataba wa rekodi wa thamani ya mamilioni ya dola, kufuatia shindano la kununua kazi yake lenye thamani ya dola milioni tatu, ripoti ya Billboard imeeleza.
Xania Monet aliundwa na Telisha Jones kutoka Mississippi, akitumia chombo cha muziki cha generative kinachoitwa Suno, kilichotungwa na Timbaland, kubadilisha mistari ya wimbo kuwa nyimbo kamili. Hatimaye, mkataba ulichukuliwa na Hallwood Media, kampuni ya burudani inayosimamiwa na mkurugenzi wa zamani wa Interscope, Neil Jacobson.
Hadi sasa, Xania tayari yupo kwenye chati za Billboard, akitawala nafasi ya 25 katika msanii anayekua pia anashika namba 1 kwenye R&B Digital Song Sales na wimbo wake unaoitwa “How Was I Supposed to Know.”