Kaka wa marehemu Emmanuel Mathias, maarufu kama MC Pilipili, amesema matokeo ya uchunguzi wa awali yanaonyesha kwamba kifo cha mdogo wake kilisababishwa na kupigwa na watu wasiojulikana, tukio lililompelekea kujeruhiwa vibaya na hatimaye kupoteza maisha.
Aidha, amesema familia imepokea taarifa hizo kwa majonzi makubwa na sasa inasubiri hatua zaidi kutoka kwa vyombo vya usalama ili kuhakikisha waliohusika wanatambulika na kuchukuliwa hatua za kisheria.