Kaka wa Diamond Platnumz Ricardo Momo amezungumza na Rick Media kuhusu sakata la Harmonize kutaka maelewano na bosi wake wa Zamani Diamond Platnumz.
Ricardo amesema kuwa "Unajua Diamond ni mzazi kwa Harmonize na kurumbana kwa mtoto na mzazi ni jambo la kawaida lipo hivyo usitegemee kugombana kwa moja kwa moja"
Ricardo ameongeza kuwa "Diamond Platnumz hana ubaya kwa Harmonize, amejaa wema hata Harmonize akimtazama Diamond akitafuta ubaya wa Diamond nafsi inamsuta. Mimi siamini kwamba vita pekee inaweza kukufanya ufanikiwe"
Mtazame hapa chini Ricardo Momo