Timu ya mawakili wa Staa wa Muziki #RKelly imetuma ombi la dharura wakitaka #RKelly atolewe haraka kwenye kizuizi cha serikali ya shirikisho na apelekwe kwenye kifungo cha nyumbani. Wanasema maisha yake yako hatarini na wametoa tuhuma nzito dhidi ya serikali kwa utovu wa nidhamu.
Katika hati ya kesi iliyowasilishwa Jumanne, ambayo Variety iliiona, mawakili wa #Kelly wamedai kuwa wana ushahidi wa kuaminika kwamba maafisa wa gereza walimshawishi mfungwa mmoja ili amuue Kelly wakati akiwa gerezani huko North Carolina, ambako anatumikia kifungo cha miaka 30.
Wamewasilisha tamko la kiapo kutoka kwa Mfungwa mwenzie na #Kelly, #MikealGlennStine ambaye alifichua kuwa maafisa walimwahidi kumwachilia huru ikiwa atamuua #Kelly katika siku zake za mwisho.
Stine alisema aliambiwa kuwa Kelly na mawakili wake walikuwa wanakaribia kufichua taarifa nzito, jambo linalohusishwa na madai kwamba maafisa walivunja haki ya siri kati ya mteja na wakili kwa kuchungulia barua binafsi.
Pia alieleza kuwa aliambiwa atashtakiwa kwa mauaji ya Kelly lakini ushahidi ungefanyiwa hila ili kuhakikisha hakutakuwapo na hukumu.