Sean Combs, maarufu Diddy, anakabiliwa na mashitaka mengi ya usafirishaji wa binadamu kwa matumizi ya ngono, miongoni mwa kesi maarufu ni Ile inayomuhusisha mpenzi wake wa zamani, Casandra "Cassie" Ventura.
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la "Jane," aliyeripotiwa kuwahi kuwa na uhusiano na Diddy kati ya mwaka 2021 hadi 2024, alisoma ushahidi wa kesi hiyo na kusema alishangaa. Alisema, "Nilijisikia kana kwamba naandika hadithi yangu mwenyewe."
Jane alielezea jinsi uhusiano wao ulivyokuwa wa kusisimua mwanzoni lakini uligeuka kuwa mgumu aliposhiriki kwenye matendo ya ngono yasiyo ya kawaida. Alieleza kuwa alijaribu kuzungumza na Diddy kuhusu matendo hayo na alihisi alidhulumiwa baada ya miaka mitatu ya kushiriki kwenye ngono na watu asiowafahamu.