Willy Paul akamatwa na Polisi nyumbani kwake siku ya leo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: willy-paul-akamatwa-polisi-nyumbani-kwake-siku-leo-777-rickmedia

Willy Paul akamatwa na polisi nyumbani kwake huko Syokimau, Kenya kufuatia taarifa za msanii huyo kumgonga mtu na gari na kutoroka eneo la tukio.

Kabla ya kukamatwa Willy Paul aliandika kupitia instagram yake kuwa; "Nimeambiwa kuna maafisa wa polisi nje ya nyumba yangu Syotani Villas wakisubiri kunikamata wakisema nilimgonga mtu na kukimbia, wanataka kuniuwa!!! Kitu kama hicho kilitokea mwaka jana. Kama kitu kitatokea kwangu mjue ni watu wamevaa sare za polisi na wako nje ya nyumba yangu sasa hivi!!!"