WINNERMAN NA DAVIDO KUTOA REMIX YA WIMBO “GIVE ME CHANCE”, KULENGA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI

-rickmedia: Rick

Rick

1 day ago
rickmedia: winnerman-davido-kutoa-remix-wimbo-give-chance-kulenga-soko-afrika-mashariki-105-rickmedia

Msanii wa muziki wa Afro-fusion kutoka Nigeria, Winnerman, ameachia remix ya wimbo wake maarufu “Give Me Chance”, akimshirikisha staa wa muziki wa Afrika, Davido, pamoja na Sabushebu.

Wimbo huo uliotayarishwa na Egar Boi, ni toleo jipya la wimbo uliofanikiwa kuwa miongoni mwa nyimbo zinazosikilizwa zaidi za Winnerman. Unazungumzia mapenzi, majuto, uvumilivu na ombi la kupewa nafasi nyingine katika mahusiano.

Toleo la awali la “Give Me Chance” lilitoka Aprili 2026 kupitia EP yake ya kwanza, Winnerman’s Universe, huku remix hiyo ikitoka rasmi Oktoba 16, 2026.

Katika kuutangaza wimbo huo, Winnerman anatarajiwa kufanya ziara ya vyombo vya habari jijini Nairobi, Kenya, kuanzia Desemba 10 hadi 15, 2026. Ziara hiyo itahusisha mahojiano na vituo mbalimbali vya redio na televisheni, vipindi vya muziki na maonesho ya moja kwa moja.

Pia, atafanya mahojiano kwa njia ya mtandao na XFM pamoja na NTV Uganda, ili kufikia mashabiki wa muziki nchini Uganda.

Mashabiki katika ukanda wa Afrika Mashariki pia watapata nafasi ya kushiriki kampeni ya “Give Me Chance Dedications”, itakayowapa fursa ya kuutumia wimbo huo kuwaombea au kuwawekea wakfu watu wanaotamani kuwapa nafasi nyingine katika mapenzi.

Wimbo wa “Give Me Chance (Remix)” unapatikana kupitia majukwaa mbalimbali ya muziki ikiwemo Spotify, Boomplay, Apple Music, Audiomack na YouTube Music.