Atayeuza 'Antibiotic' bila cheti cha Daktari kupelekwa Mahakamani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: atayeuza-antibiotic-bila-cheti-cha-daktari-kupelekwa-mahakamani-803-rickmedia

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa Wafamasia na Wamiliki wa Maduka ya Dawa wanaouza Dawa za ‘Antibiotic’ bila Wateja kuwa na Cheti cha Daktari kwa kuwa kufanya hivyo ni kuendeleza tatizo la Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha Afya za watu.

Akizungumza katika Kongamano la Tatu la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa Mkoani Arusha, Novemba 17, 2023 amesema “Waganga Wakuu wa Mikoa fanyeni kaguzi za kushtukiza, tumeni watu wakanunue dawa, ukipata ushahidi mara tatu unasubiri nini? Wananchi hawatuelewi tunapounda Tume Tume Tume.”

Wiki kadhaa zilizopita Mfamasia kutoka Wizara ya Afya, Neema Nagu aliiambia JamiiForums mgonjwa akipata madhara ya dawa aliyopewa bila Cheti cha Daktari, Mfamasia atawajibishwa kulingana na Kanuni za Baraza la Famasia.