Mfalme Charles III agundulika kuwa na Saratani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 months ago
rickmedia: mfalme-charles-iii-agundulika-kuwa-saratani-983-rickmedia

Mfalme Charles III amekutwa na Ugonjwa wa Saratani baada ya kufikishwa Hospitali kwaajili ya kufanya Vipimo vya Afya.

Taarifa ya Idara ya Mawasiliano ya Kasri la Kifalme imesema, Madaktari wamemshauri Mfalme asitishe kwa muda shughuli za Umma ili kuanza Matibabu ingawa ataendelea na majukumu mengine ya Kiserikali.

Pia, Mfalme amesema, amechukua uamuzi wa kutangaza taarifa ya Ugonjwa ili kuondoa sintofahamu na uzushi unaoweza kuenezwa pamoja na kuongeza uelewa kwa waathiriwa wa Saratani.