Loading...

Mganga Mkuu wa Mkoa "Watoto wanaozaliwa Dar kwa siku ni zaidi ya 430

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: mganga-mkuu-mkoa-watoto-wanaozaliwa-dar-kwa-siku-zaidi-430-523-rickmedia

Imeelezwa wastani wa Watoto wanaozaliwa Mkoani Dar es Salaam kwa Siku ni zaidi ya Watoto 430 ambapo 86 kati yao sawa na 20% wanahitaji Huduma za Watoto Wachanga wenye matatizo mbalimbali.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mohammed Mang’una, amesema Vituo vya Serikali vinavyotoa Huduma ya Uzazi ni 136, kati ya hivyo 30 vinatoa Huduma za Upasuaji na 7 ndio vinatoa Huduma ya Watoto Wachanga wenye matatizo mbalimbali hali inayosababisha msongamano vituoni na kuhatarisha Maisha ya Watoto wachanga.

Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Mpango wa NEST360 (Newborn Essential Solutions and Technologies) Nchini katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, ambapo NEST360 imeeleza kiwango cha sasa cha vifo vya Watoto Wachanga ni 24 kwa kila Watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai