Rais wa Kenya, William Ruto amesema Serikali inafanya mabadiliko ya gharama za matibabu kwa Wananchi wa kipato cha chini wanaotumia Bima za Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF) ambapo kuanzia Janauari 1, 2024 waliokuwa wanalipa Tsh. 8,201 kwa mwezi wataanza kulipa Tsh. 4,921.
Ruto ameongeza kuwa kwa Wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo, Serikali inakamilisha mpango wa kutambua hali ya kipato cha kila Mwananchi na itabeba gharama zote ili watibiwe bure.
Amesema "Kila Mwananchi kwa umoja wetu tutaenda Hospitali na tutatibiwa bila ya kuulizwa Pesa yoyote kwasababu tunataka kuhakikisha kwamba Kenya ni Nchi ya Usawa"
Utekelezaji wa mpango huo unatokana na Kenya kupitisha Sheria ya Fedha inayotaka kila mfanyakazi kukatwa 2.75% ya Mshahara kila mwezi ili kuchangia gharama za uendeshaji wa NHIF.