Mamlaka ya #Seoul imesema Korea Kusini inapanga kuanzisha marufuku ya ulaji wa nyama ya mbwa ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Ulaji wa nyama ya mbwa haujakatazwa waziwazi wala haujahalalishwa nchini Korea Kusini, na serikali zilizofuata zimeshindwa kuendeleza ahadi za kukomesha tabia hiyo.
Sheria hiyo maalum itaruhusu kipindi cha miaka mitatu kumaliza tabia hiyo. Ikiwa mswada huo utapitisha bunge kabla ya mwisho wa mwaka, marufuku ya nyama ya mbwa itaanza kutekelezwa kikamilifu mnamo 2027.