Loading...

Afisa Maliasili na Mwenyekiti wa kijiji Iringa kizimbani kwa ubadhirifu wa Fedha

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 months ago
rickmedia: afisa-maliasili-mwenyekiti-kijiji-iringa-kizimbani-kwa-ubadhirifu-fedha-97-rickmedia

Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Mufindi, Jeswald Gustav Ubisiambali na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapanda, Oberd Francis Madembo, wamefikishwa Mahakamani kwa mashtaka mawili.

Shtaka la kwanza ni Ubadhirifu na ufujaji na la pili wakiwa Watumishi wa Umma walifanya Wizi wa Tsh. 19,970,000 mali ya Kijiji cha Mapanda kilichopo Wilaya ya Mufindi

Washtakiwa walikana makosa yao na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 13, 2023. Kwa kuwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana wamepelekwa mahabusu.