Askofu wa zamani ahukumiwa kifungo cha miaka 6 kwa kosa la ubakaji

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

19 hours ago
rickmedia: askofu-zamani-ahukumiwa-kifungo-cha-miaka-kwa-kosa-ubakaji-549-rickmedia

Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki nchini Australia, Christopher Saunders, amehukumiwa kifungo cha miaka 6 na nusu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kuwanyanyasa kingono vijana wawili wa jamii ya Waaborijino.

Saunders, mwenye umri wa miaka 76, alijiuzulu kuwa Askofu wa Broome mwaka 2020 baada ya tuhuma hizo kuibuka. Mahakama ilielezwa kuwa aliwakaribia vijana hao kwa kuwapa pombe, fedha na kuwakaribisha katika mikusanyiko ya “shirts-off”, huku akitumia pia mali za Kanisa.

Alipatikana na hatia ya kosa moja la ubakaji na makosa 12 ya shambulio la aibu. Anaweza kuomba kuachiliwa kwa masharti mwezi Februari 2031.

Saunders anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wa juu zaidi wa Kanisa Katoliki duniani kuwahi kufikishwa mahakamani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.