Jaji wa UN akutwa na hatia ya kumshitaki mtu bila haki

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: jaji-akutwa-hatia-kumshitaki-mtu-bila-haki-301-rickmedia

Jaji wa Umoja wa Mataifa kutoka Uganda, Lydia Mugambe, amepatikana na hatia na Mahakama ya Oxford Crown Alhamisi Machi 13, 2025, kwa kumlazimisha msichana kumfanyia kazi kama mtumwa.

Mugambe, aliyewahi kuwa mshirika wa Taasis ya Mafunzo ya Haki za Binadamu kwenye Chuo Kikuu cha Columbia, alimshawishi msichana huyo kusafiri hadi Uingereza kwa ahadi za uongo. Hata hivyo, alipowasili, alitumiwa kama mfanyakazi wa ndani bila malipo huku akinyimwa uhuru wake wa msingi.

Hukumu yake inatarajiwa kutolewa Mei 2, 2025.