Lupita Nyong'o anaungana na Maelfu ya Wakenya kupinga Muswada wa Fedha 2024 wa nchi hiyo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: lupita-nyongo-anaungana-maelfu-wakenya-kupinga-muswada-fedha-2024-nchi-hiyo-948-rickmedia

Mrembo na Mwigizaji kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong'o amewaunga mkono vijana (Gen Z) waliojitokeza kwenye maandamano siku ya jana maalum kabisa kwaajili ya Muswada wa Fedha 2024 ambao wanaona una makosa.

Lupita ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akitumaini Serikali ya nchi hiyo itasikiliza ombi hilo la wananchi na kulifanyia kazi, Lupitia alimaliza kwa kuunga mkono kampeni ya #RejectFinanceBill2024

Japo maisha yake kwasasa yapo Marekani zaidi lakini Lupita amekuwa mstari wa mbele kusapoti chochote ambacho kinaleta maendeleo nyumbani kwao (Kwenye asili yake) Kenya na wanachi wa Kenya siku zote wamekuwa wakimshukuru kwa hilo.