M23 Waanzisha Vurugu tena DRC,wauteka Mji wa Nyabibwe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: m23-waanzisha-vurugu-tena-drcwauteka-mji-nyabibwe-186-rickmedia

Zikiwa zimepita siku mbili tangu waasi wa Kundi la M23 watangaze kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakitaja sababu ni kuwepo janga la kibinadamu, waasi hao wameibuka na kuuteka mji wa Nyabibwe ulioko Jimbo la Kivu Kusini nchini humo.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti leo Alhamisi Februari 6, 2025, kuwa M23 wameibuka na kuukamata Mji wa Nyabibwe ulioko kwenye ukingo wa Ziwa Kivu, Jimbo la Kivu Kusini nchini DRC.

Mji wa Nyabibwe uko takriban Kilometa 70 kutoka Mji wa Bukavu, mji ambao awali waasi hao walitangaza kuwa hawana nia ya kuuteka na kuuweka chini ya himaya yao.

Vyanzo vinane vya habari wakiwemo wafanyakazi wa mashirika ya kuhudumia jamii eneo la Nyabibwe wamethibitisha mji huo kutwaliwa na waasi wa M23.