Mtu mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Kisa Sh 5,000

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 years ago
rickmedia: mtu-mmoja-auawa-kwa-kuchomwa-kisu-kisa-5000-785-rickmedia

Abubakari Ibrahim mwenye umri wa miaka 21 , Mkazi wa katunda auawa kwa kuchomwa na kisu na kijana mwenzake katika eneo la machinjio wilaya, mkoa wa Geita 

Tukio hili limethibitishwa na mkuu wa kituo wa Geita ambaye alisema kwamba Abubakari alikuwa akidai deni la shilingi elfu tano (5000) baada ya kazi ya kuchinja na kuchuna mifugo katika machinjio ya serikali kata ya Mtakuja  

"Walikuwa wakidaina deni la shilingi elfu tano baada ya kazi ya kuchinja na mifugo ambayo ilichinjwa yaani hawa ni wachunaji wako pale machinjioni kama wachunaji kwahiyo baada ya malipo ndio wakaanza kugombania iyo elfu tano "

Mtumiwa anashikiliwa na Jeshi la polisi huku upelelezi ukiendelea juu yake.




(Imeandaliwa na Ibrahim Jafari)