Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema matukio ya Utapeli unaofanywa na Wahalifu wanaotuma jumbe za 'Ile Pesa Tuma Kwa Namba Hii' umepungua kulinganisha na kipindi ambacho hakukuwa na Usajili wa Laini za Simu.
Akizungumza kupitia CloudsFM, Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma kutoka TCRA, Rolf Kibaja, amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa Laini za Simu tofauti ipo kubwa. Ukiangalia takwimu za Septemba Laini ziliripotiwa kwa uhalifu na utapeli ni 16,000 wakati ripoti iliyopita ilikuwa ni laini 22,000.
Ameongeza kuwa kadri Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wanavyoripoti namba zote zinazohusika na matukio ya Uhalifu na Utapeli kwenda 15040, namba hizo zinashughulikiwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia.