Loading...

Waandamanaji Senegal washinikiza uchaguzi ufanyike ndani ya wiki moja

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: waandamanaji-senegal-washinikiza-uchaguzi-ufanyike-ndani-wiki-moja-465-rickmedia

Mamia ya Waandamanaji wameripotiwa kuendelea na maandamano ya kumshinikiza Rais #MackySall kufanya Uchaguzi Mkuu ndani ya mwezi mmoja kabla ya muda wa Urais wake kumalizika Aprili 2, 2024.

Maandamano hayo yameendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja ikiwa ni tangu Rais Sall atangaze kuahirisha Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 25, 2024 na badala yake kusogeza mbele hadi Desemba 15, 2024, muda ambao ulibatilishwa na Baraza la Katiba.

Baadhi ya madai ya Waandamanaji ni kuachiwa kwa Kiongozi wa Upinzani, Ousmane Sonko. Wiki iliyopita, Rais Sall aliunda kikosi cha Maridhiano ambacho kilipendekeza Uchaguzi ufanyike Juni 2024, hata hivyo Upinzani umegomea pendekezo hilo.