Kikosi cha Kanda ya Afrika Mashariki kimeanza kuondoka eneo lenye machafuko lililopo Mashariki mwa DRCongo baada ya wenyeji kudai Jeshi hilo halifanyi kazi iliyowapeleka eneo husika kama inavyotakiwa.
Awali, Wanajeshi hao waliwasili eneo husika Novemba 2022 wakiitikia wito wa maombi ya Serikali ya DRC kusaidia udhibiti wa kundi la waasi la M23
Wanajeshi 100 wa Kenya wameonekana Uwanja wa Ndege wa Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini wakianza safari ya kuondoka ikiwa ni siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba 20, 2023.