Loading...

Wanakijiji 170 waripotiwa kuchinjwa ndani ya wiki moja huko Burkina Faso

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: wanakijiji-170-waripotiwa-kuchinjwa-ndani-wiki-moja-huko-burkina-faso-437-rickmedia

Takriban Watu 170 kutoka Vijiji vya Komsilga, Nodin, na Soro katika Mji wa Yatenga, wameripotiwa kuuawa na Waasi wanaohusishwa na Vikundi vya al Qaeda na IS.

Taarifa iliyotolewa jana na Mwendesha Mashtaka wa Serikali leo Machi 3, 2024 imeeleza kuwa mauaji hayo yaliyoanza Wiki iliyopita yalihusisha Watu 17 waliokutwa Kanisani na maeneo mengine ya mikusanyiko katika Vijiji hivyo.

Amesema tayari uchunguzi wa kina umeanza juu ya tukio hilo ambalo ni mwendelezo wa matukio ya Ukatili na Unyanyasaji unaotajwa kuhusisha masuala ya Kidini ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko na vifo kwa zaidi ya miaka 10 ikiwemo Watu zaidi ya Milioni 2 kuyakimbia makazi.

-