Leo February 24,2026 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan amefanya uzinduzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ukinzi wa Taifa huko Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo, Rais Samia alisema uwekezaji huo unaimarisha uhuru wa maamuzi ya taifa na kulipa heshima katika masuala ya ulinzi barani Afrika, akibainisha kuwa Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi zilizotoa kipaumbele cha juu kwa shughuli za ulinzi.
Rais Samia alieleza kuwa katika mazingira ya sasa ya usalama wa dunia, ulinzi hauhusiani na silaha pekee, bali unategemea pia upatikanaji na uchambuzi wa taarifa, matumizi ya teknolojia za kisasa, mifumo madhubuti ya mawasiliano pamoja na ubobezi wa hali ya juu wa kitaalamu.
Sambamba na hilo Rais Samia, kama Amiri Jeshi Mkuu, aliahidi kuhakikisha kuwa awamu zilizobaki za mradi huo zinakamilishwa kwa wakati ili kuendelea kuimarisha uwezo wa taifa katika kulinda mipaka, maslahi na usalama wa nchi.