Dk Emmanuel Nchimbi kuanza Ziara Mikoa 5

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: emmanuel-nchimbi-kuanza-ziara-mikoa-610-rickmedia

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi leo Jumatano, Mei 29,2024 anaanza ziara katika mikoa mitano ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 na kuimalisha chama ambapo atafanya mikutano mbalimbali ya ndani na ya hadhara.

Katika ziara hiyo, Dk Nchimbi ataambatana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Mambo ya Nje, Rabia Abdallah.

Kwenye ziara hiyo, viongozi hao watapata fursa ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.