Rais Mstaafu ahukumiwa Maka 5 Jela kwa mashtaka ya Ufisadi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: rais-mstaafu-ahukumiwa-maka-jela-kwa-mashtaka-ufisadi-421-rickmedia

Mohamed Ould Abdel Aziz aliyekuwa Rais wa Taifa hilo kati ya mwaka 2008 hadi 2019 amekutwa na hatia ya kujipatia mali kwa njia za haramu ikiwemo ubadhirifu

Mstaafu huyo na Viongozi wengine 10 wakiwemo waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu walikuwa wanachunguzwa kwa tuhuma za kumiliki utajiri usio halali, matumizi mabaya ya madaraka, kuendesha biashara Serikalini na Utakatishaji Fedha.

Mahakama imeamuru Mali za Kiongozi huyo zilizopatikana kwa njia za Rushwa zitaifishwe ikiwemo Kiasi cha Tsh. Bilioni 180 ambazo alituhumiwa kuzipata kupitia miradi ya Rushwa aliyoshiriki akiwa Rais

Tuhuma za ufisadi dhidi ya Aziz ziliibuliwa Bungeni mwaka 2020 ambapo alidaiwa kujipatia sehemu ya Kodi za Uchimbaji Mafuta, Uuzwaji wa Mali za Umma na Rushwa kutoka kampuni za China zilizopata zabuni za kusambaza vyakula.