Taliban Wapiga Marufuku Mwanamke Kusikia Sauti Ya Mwanamke Mwenzie

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 month ago
rickmedia: taliban-wapiga-marufuku-mwanamke-kusikia-sauti-mwanamke-mwenzie-35-rickmedia

 Kundi la Taliban ambalo limejikita kama watawala wa Afghanistan, miaka mitatu baada ya kunyakua mamlaka mwaka 2021 limeweka sheria mpya kwa Wanawake wa Afghanistan.

Taliban imesema ni marufuku kwa Mwanamke kusali kwa sauti kubwa au kusoma Quran mbele ya wanawake wengine, kulingana na waziri wa serikali ya Taliban

Marufuku ya hivi punde Khalid Hanafi, waziri wa maadili wa Taliban, amesema ilikuwa ni marufuku kwa wanawake watu wazima kuruhusu sauti zao kusikika, kwa mujibu wa The Associated Press.

Wakati wa hafla katika mkoa wa Logar mashariki siku ya Jumapili, Makamu na Waziri wa Uadilifu Khalid Hanafi alisema:

"Ni marufuku kwa mwanamke mzima kusoma aya za Qur'ani au kufanya kisomo mbele ya mwanamke mwingine mzima. Hata nyimbo za takbir (Allahu Akbar) haziruhusiwi.