TikTok wanakabiliwa na Kutokutunza Falagha za Watoto Marekani

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 months ago
rickmedia: tiktok-wanakabiliwa-kutokutunza-falagha-watoto-marekani-311-rickmedia

Tume ya Biashara ya Shirikisho la Marekani (FTC) imepeleka malalamiko dhidi ya TikTok na kampuni mama ya China ya ByteDance kuhusu ukiukaji unaowezekana wa faragha ya watoto kwa Idara ya Haki (DOJ).

FTC inasema uchunguzi wake umefichua sababu ya kuamini kwamba makampuni yanakiuka au yanakaribia kukiuka sheria.

Katika taarifa kwa BBC News, msemaji wa TikTok alisema wamesikitishwa na uamuzi huo.

Kesi hiyo ni tofauti na sheria iliyopitishwa mapema mwaka huu ya kupiga marufuku TikTok nchini Marekani ikiwa ByteDance haitauza biashara hiyo.

Mdhibiti alisema uchunguzi wake ulilenga ukiukaji unaoweza kutokea wa Sheria ya FTC na Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA).

FTC pia ilisema huwa haitangazi kwamba imepeleka malalamiko kwa DOJ lakini katika hali hii ilihisi kufanya hivyo ni kwa manufaa ya umma.

COPPA inasimamia ukusanyaji, matumizi na ufichuaji wa taarifa za kibinafsi na huduma za mtandaoni kuhusu watoto walio na umri wa chini ya miaka 13.

Sheria ya FTC inalenga "vitendo au desturi zisizo za haki au za udanganyifu" za makampuni.

Kujibu, msemaji wa TikTok alisema kampuni hiyo haikubaliani na madai hayo na kwamba "imekuwa ikifanya kazi na FTC kwa zaidi ya mwaka mmoja kushughulikia wasiwasi wake."

"Tumesikitishwa na shirika hilo kutafuta kesi badala ya kuendelea kufanya kazi nasi kupata suluhisho la kuridhisha," waliongeza.

Msemaji wa DOJ aliiambia BBC News "hawawezi kutoa maoni yao kuhusu kiini cha rufaa kutoka kwa FTC dhidi ya TikTok."

"Kulingana na mtazamo wetu wa kawaida, Idara ya Haki ilishauriana na FTC kabla ya rufaa hii na itaendelea kufanya hivyo tunapozingatia madai," waliongeza.

Tangazo la FTC linaongeza shinikizo linalozidi kuongezeka la TikTok nchini Marekani.

Mnamo Aprili, Rais Joe Biden alitia saini kuwa sheria mswada ulioipa ByteDance muda wa juu zaidi wa mwaka mmoja kuuza programu au kupigwa marufuku nchini.

Hiyo ina maana kwamba tarehe ya mwisho huenda ikafika muda fulani mwaka wa 2025, baada ya mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2024 kuchukua madaraka.

Sheria ilianzishwa ili kushughulikia wasiwasi kwamba TikTok inaweza kushiriki data ya mtumiaji na mamlaka ya China - madai ambayo kampuni imekanusha.