Uhuru Kenyatta aitaka Serikali ya Ruto kupiga kazi na sio kulaumu Utawala uliopita

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: uhuru-kenyatta-aitaka-serikali-ruto-kupiga-kazi-sio-kulaumu-utawala-uliopita-520-rickmedia

Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameiambia Serikali iliyoko Madarakani iache kuulaumu Utawala wake kwa kushindwa kutimiza malengo iliyowaahidi Wananchi

Uhuru amesema “Kila mara Mtu anaposhindwa kufanya anachopaswa kufanya, analaumu Serikali iliyopita. Huu mwenendo hata kama Mke amekataa kujifungua, tutalaumiwa sisi, lakini tumezoea hili.”

Mapema Mwezi huu, Waziri wa Fedha, Profesa Njuguna Ndung’u aliilaumu Serikali iliyopita kwa chanzo cha gharama kubwa za Maisha. Wiki iliyopita, Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkomen naye aliilaumu Serikali iliyopita kwa Ujenzi wa Paa linalovuja katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.