Al Ahly yakamiisha makundi kwa kuipiga Yanga 1-0

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: ahly-yakamiisha-makundi-kwa-kuipiga-yanga-1-0-66-rickmedia

Timu ya Yanga imekamilisha Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupoteza kwa goli 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya #AlAhly ya Misri katika mchezo wa Kundi D

Goli pekee limefungwa na Hussein El Shabat dakika ya 46, hivyo kuiwezesha Al Ahly kufikisha pointi 12 ikifuatiwa na Yanga yenye alama 8, sawa na CR Belouizdad ambayo imemaliza Makundi kwa kuifunga Medeama (4) magoli 3-0.

Hatua ya Robo Fainali inatarajiwa kuanza Machi 29, 2024 ambapo Yanga inatarajiwa kucheza na moja kati ya timu itakayoongoza Kundi.