Pamoja na kuweka wazi kuwa hakutamani kupoteza pambano lake alilokuwa akilisubiri kwa muda mrefu kwenye mahojiano tuliyofanya naye hapa Rick Media lakini Bondia Karim Mandonga amepoteza pambano hilo dhidi ya Bondia Mada Maugo kwa kupigwa katika Raundi ya 6 kwa TKO kwenye pambano lililofanyika Mkoani Morogoro.
Ngumi iliyopigwa kwenye kidevu katika pambano hilo la Raundi 6 ilimfanya Mandonga apoteze mwelekeo, ndipo mwamuzi Pendo Njau akaingilia na kumaliza pambano
Baada ya pambano, Maugo amesema “Mwalimu wangu ambaye ni mke wangu aliniambia niwe na utulivu ulingoni, hilo nimelitimiza, nikikutana na Mandonga popote pale bado nitampiga tena.”
Upande wa Mandonga amesema “Maugo hawezi kunisumbua, ni mchezo tu, uwezo wa kunipiga hana.”