Kesi ya Mkude, METL kusikilizwa 27 Novemba Mwaka huu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: kesi-mkude-metl-kusikilizwa-novemba-mwaka-huu-811-rickmedia

Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kusikiliza usuluhishi katika kesi ya kiungo wa Yanga, Jonas Mkude ambaye anaidai Kampuni ya Mohamed Enterprises (T) Limited (METL) fidia ya Sh1 bilioni kwa kutumia picha yake katika matangazo ya biashara ya bidhaa zake bila idhini yake.

Kesi hiyo ya madai namba 192 ya mwaka 2023 imetajwa leo Novemba 20, 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip na imepangwa kusikilizwa kwa hatua ya usuluhishi Novemba 27, 2023.

Mbali ya kudai fidia hiyo, Mkude ameiomba mahakama hiyo iiamuru kampuni hiyo kumlipa mrabaha unaotokana na manufaa ambayo kampuni hiyo imeyapata.