Simba Yaanza kupangua Benchi lake la Ufundi yaanza kuwapunguza hawa...

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 years ago
rickmedia: simba-yaanza-kupangua-benchi-lake-ufundi-yaanza-kuwapunguza-hawa-889-rickmedia

Klabu ya Simba imeanza kudili na Benchi lake la ufundi kwa wapuguza baadhi ya watu akiwemo Kocha wao wa Magoli kipa Chlouha Zakaria aliefanya kazi ndani ya simba kwa miezi 7,Kelvin Mandla na Fareed Cassim ambae alikuwa mtaalamu wa viungo.

Kupitia kurasa za mitandao za Simba amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika

"Shukrani kwa mtaalamu wa viungo Fareed Cassim kwa muda wote aliokuwa nasi kuhakikisha anawatibu wachezaji wetu. Tunasema asante."

"Asante kwa Kelvin Mandla ambaye alikuwa kocha wetu wa viungo. Tunakushukuru kwa muda wote uliokuwa nasi."

"Asante kocha wetu wa magolikipa, Chlouha Zakaria kwa muda wote uliokuwa sehemu ya benchi letu la ufundi. Tunakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya nje ya Simba."