Loading...

Ujerumani, Scotland kufungua Michuano ya Euro 2024 leo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: ujerumani-scotland-kufungua-michuano-euro-2024-leo-835-rickmedia

Michuano ya Kombe la Euro inaanza leo nchini Ujerumani, huku mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa ikiwa kati ya Ujerumani na Scotland kuanzia saa 4 usiku.

Hii ni mechi ya Kundi A ambayo itaanza kwa kuonyesha picha halisi ya michuano hiyo msimu huu itakavyokuwa ikiwa inapigwa kwenye Uwanja wa kisasa wa Munich Football Arena.

Ujerumani ni kati ya taifa ambalo limefanya vizuri kwenye michuano hii ikiwa imeshatwaa ubingwa mara tatu ikiwa sasa inakwenda kuutafuta kwa mara ya nne ikiwa kwenye aridhi ya nyumbani.

Kocha kijana Julian Nagelsmann hakuanza vizuri kikosi hicho, lakini baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo dhidi Ufaransa na Uholanzi kwenye michezo iliyopigwa mwezi Machi imeanza kuonyesha mwanga halisi wa kikosi hicho.

Hata hivyo Scotland imetengeneza kikosi chake baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michezo ya kufuzu baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya mataifa makubwa Hispania, Norway na Georgia.