Waendesha Mashtaka wataka Dani Alves aongezwe miaka ya kukaa jela

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 months ago
rickmedia: waendesha-mashtaka-wataka-dani-alves-aongezwe-miaka-kukaa-jela-198-rickmedia

Waendesha Mashtaka wa Uhispania waliosimamia kesi dhidi ya beki wa zamani wa Barcelona, Dani Alves wamedai kifungo cha Miaka Minne na Nusu gerezani alichohukumiwa ‘staa’ huyo kwa tuhuma za Unyanyasaji wa kingono ni kidogo na anastahili kuongezewa adhabu.

Wanatarajia kukata rufaa ili nyota huyo wa zamani wa Seville, Juventus, Paris Saint-Germain na Sao Paulo ambaye pia ametakiwa kumlipa Mshtaki Pauni 128,000 (Tsh. Milioni 411) kama fidia, aongezewe kifungo kiwe Miaka 9 hadi 12.

Alves (40) ambaye amesomewa hukumu Februari 2024 kutokana na tukio lililoelezwa kutokea kwenye Ukumbi wa Muziki, ameshikiliwa tangu Januari 2023 japo alipinga na kudai alishiriki ngono na Mshtaki baada ya Wawili hao kukubaliana.