Cassie Adai Diddy Alimbaka Kipindi yupo na Mahusiano na Mume wake wa Sasa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 month ago
rickmedia: cassie-adai-diddy-alimbaka-kipindi-yupo-mahusiano-mume-wake-sasa-335-rickmedia

Mengine mapya kutoka kwenye ushahidi wa #CassieVentura katika kesi dhidi ya #Diddy, Ameiambia mahakama kwamba #Diddy alimbaka kwenye sakafu ya nyumba yake baada ya wao kuachana na baadaye alijaribu kujiua kwa sababu hakuweza kuvumilia maumivu yote.

Mwimbaji huyo alitoa ushahidi kwamba mnamo Agosti 2018 walikuwa na mazungumzo ya kufunga ukurasa wa uhusiano wao walikutana kwenye mgahawa huko Malibu, ambako #Diddy alikuwa mpole, mcheshi na wa kimapenzi. Alisema Diddy alimuendesha hadi nyumbani kwake na akamlazimisha kufanya nae ngono.

#Cassie aliambia mahakama kuwa macho ya #Diddy yalibadilika na kuwa meusi alipombaka kwenye sakafu ya sebule ya nyumba yake. Alieleza kuwa alikuwa analia lakini #Diddy aliendelea kumbaka, alimalizia ndani yake, kisha akainuka na kuondoka.

#Cassie aliwaambia majaji kuwa ubakaji huo ulitokea wakati alikuwa kwenye uhusiano na #AlexFine ambaye sasa ni mume wake.

Alitoa ushahidi kwamba walifanya ngono tena mara moja baada ya kubakwa, lakini wakati huo ilikuwa kwa hiari.

Alipoulizwa na upande wa mashtaka kwa nini alikubali kufanya ngono kwa hiari na mtu aliyembaka hapo awali, #Cassie alisema ni kwa sababu walikuwa kwenye uhusiano kwa miaka 10.