Chella anazidi kuonyesha ukuaji wake kwenye 'Chella Chant EP'

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: chella-anazidi-kuonyesha-ukuaji-wake-kwenye-chella-chant-ep-898-rickmedia

Kwa miaka kadhaa msanii kutoka Nigeria, Chella amejiimarisha na anajulikana kama mmoja wa watu wenye hisia kali,sauti za kukusudia katika wimbi jipya la muziki wa Kiafrika. Kuanzia nyimbo zake za mwanzo kipindi anaanza muziki mpaka sasa kwenye kazi zake mpya "Chella Chant EP".

Hii imeonyesha ukuaji wa sauti na kimkakati, na kuvutia wasikilizaji kwa kutoka moyoni mwake namna anahadithia hadithi kupitia nyimbo zake.

Nyimbo za mwanzo za Chella ziliweka rekodi mbalimbali kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikilizaia muziki yenye nguvu kubwa duniani.

Ukubwa wa nyimbo zake za mwanzo ulichochewa na maashabiki mbalimbali kutumia nyimbo zake (Kufanya Challenge) mitandaoni hasa mtandao wa Tiktok, nyimbo zake ziliwapa ushawishi mkubwa watengeneza maudhui kuzitumia kutokana na uzuri wa nyimbo zake.

Uwezo wake wa muziki na kushirikiana na mashabiki umemkuza Zaidi mpaka kumfikisha kwenye majukwaa makubwa ikijumuisha ushindi wa AFRIMA.

Ushindi wa AFRIMA ulliimarisha zaidi uaminifu na ushawishi wake katika bara zima la Afrika Sifa hiyo ilimweka kama msanii anayechipukia na mwenye sauti ya ubunifu inayounda muziki wa kisasa wa Kiafrika.

Kupitia EP yake (Chella Chant) Iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana inayozidi kufanya vizuri, inathibitisha thamani yake kwenye muziki. EP ina jumla ya nyimbo 7 huku "My Darling" na "Loyal" zikiwa zinakamilisha idadi hiyo. humo ameshirikiana na waandaji wa muziki (Producers) mbalimbali kama Gstickz (mtayarishaji wa “My Darling”), Azed aliyeshinda tuzo, na Ragee. Together, hawa ni watayaishaji ambao wanazingatia vitu vingi katika kutayarisha kazi hivyo hutoa kazi zenye ubora.

Nyimbo zingine maarufu kwenye EP ni pamoja na "Seedy","Shameless Devil" na "Shake Am" kila moja ikitoa taswira ya kipekee ya maono ya kisanii ya Chella, EP inazingatia mada kuu za ukuaji, upendo na muunganisho.

Itoshe kusema Chella ni msanii anayetazamiwa kuja kufanya makubwa kwenye muziki wa Afrika na wengi wenye maono ya mbali kwenye kiwanda cha burudani wanasema kuwa Chella atakuja kuwa ni mmoja kati ya wasanii A-List wa balani Afrika hivyo asipuuzwe.

Je na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoisubiri kazi ijayo ya Chella baada ya Chella Chant EP?