Harmonize ameamua akate mzizi wa fitna na kuweka wazi kuwa atamuoa Kajala Masanja mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, hii ni mara baada ya Mwijaku kupost na kumshauri kuwa kama kweli anampenda Kajala basi achague moja kati ya kumuoa au kumruhusu arudi kwake mpaka mwezi mtukufu wa Ramadhan uishe.
Harmonize aliweka ahadi hiyo kwenye uwanja wa maoni (Comments) kwenye post ya Mwijaku aliyokuwa akimshauri kuhusu mambo ya dini.

Harmonize ambaye alimvisha pete ya uchumba Kajala kwa mara ya pili 29/12/2025 amekiri wazi kuwa wao hawaishi pamoja na taratibu za kumvuta Kajala kama mke zinaendelea ila kwasasa ameanza kwa kumbadili jina na kumpa jina la kiislam kwahivyo kwasasa Kajala anaitwa Swalha AbddulKahal (amechukuwa na jina la Harmonize mwishoni)
Kajala ni mkristu mzuri sana ambaye mara kadhaa amekuwa akionyesha kwenye mitandao yake ya kijamii akienda kanisani (Kanisa Katoliki), swali ni je Kajala atabadili dini na kuwa muislam kama ambavyo Marioo alidai kuwa Paulah (Mtoto wa Kajala) atabadili dini kumfuata ili waoane?