Rapa Conboi atangaza kuachana na matumizi ya pombe na bangi ili ajiboreshe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: rapa-conboi-atangaza-kuachana-matumizi-pombe-bangi-ili-ajiboreshe-308-rickmedia

Rapa Conboi ametangaza rasmi kuachana na matumizi ya bangi pamoja na unywaji wa pombe, akieleza kuwa amekuwa akijitathmini na kujifunza kujizuia tangu alipokaribia mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Amesema kuwa hatua hiyo haishii ndani ya Ramadhan pekee, bali ameazimia kuendelea nayo hata baada ya mwezi huo kumalizika, akimaanisha ameacha kabisa tabia hizo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram amepost video akizungumza kuhusu uamuzi wake, Conboi amesema:

“Kila mtu anajua nimekuwa nikivuta bangi sana na kunywa pia. Lakini nimeanza kupunguza kwa muda ili nijiboreshe, nijiboreshe pia mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa Ramadhan inaingia, nimeamua kuacha kabisa. Sitavuta wala kunywa kuanzia mwezi huu na kuendelea.”

Mbali na hilo, msanii huyo amewahimiza vijana wanaotumia vilevi na dawa za kulevya kuacha tabia hizo, akiwataka kuzingatia afya zao na kujenga maisha bora kwa siku zijazo.