Msanii wa Muziki #GigyMoney Amemvulia uvivu Mwanaharakati wa kwenye mitandao #MangeKimambi akimuita mtu ambae anaonea wanyonge kwa kuweka maudhui Yao ya Aibu kwa maslahi yake binafso bila kujali Utu wa mtu.
Mbali Na hivyo Pua Amegusia juu ya video ambayo aliwahi kushare kwenye App yake ya kipindi #ProffesorJay akiwa Maituti Hospital Na kumtabiria kifo.
"Huyu anaegeuza maumivu na AIBU ZA WATU kuwa content ndio mumuite mwanaarakati? Kweli ameweza kuwapumbaza, kama kweli anapenda haki mbona APP YAKE ANAONEA WANYONGE MATAJIRI ANAWAACHA?anatuweka akina sisi ambao atuna uwezo, matajiri anawablackmail wakishampa ela anawatoa, aliwai kumuweka mkuu mmoja wa benki kumjambisha kisha kamtoa baada ya muda, kilichotokea atujui, alimuweka pia video ya waziri mmoja baada ya muda akaitoa, ila Gigy cna cha kumpa ameanika utupu wangu bila kujali nina mtoto wala kesho yangu, hadi Mama mzazi wa star mtu mzima kamuweka na kumdhalilisha faraga yake kwakuwa tu hana cha kumpa, hajajali zamani alikuwa na mausiano nae mazuri tu ata kumkabidhi mtoto wake, Kaka yetu Prof alikuwa mgonjwa anapigania uhai, in the name of content hakumuurumia yeye wala familia yake akampost akiwa wodini na mipira na kusema hana muda mrefu wa kuishi kama vile yeye ni MUNGU!! huyu ana utu huyu? mbona nae mnafki tu, ata iyo serikali nina mashaka kuna seemu hawakukubali ushetani wake wa App ndiomana akawageuka, mbona mwanzo alikuwa anasapoti mpaka pale alipofungiwa App yake Bongo ndio akaanza kuona mabaya ya serikali? Mange we ni SHETANI, ila wachache wenye macho ya rooni ndio watakuona, MUNGU kakupa nguvu kubwa ya ushawishi unayoitumia KUVUNJA WATU, mwisho wako sio mzuri, MIMI sikusapoti sbb najua yote unatengeneza kwa faida yako, huna uchungu na nchi, FUNGUENI macho wabongo huyu malaya anatutumia, nyuma ya NAPIGANIA WATANZANIA anafanya kazi kubwa ya giza sio kwa ajili ya kubadilisha Dunia ila kuitawala, coz kaona wabongo wengi wajinga, nyinyi ndo mnampa ela lzm atengeneze kitu cha kujifanya mkombozi wenu ili mumuamini, Huyu akipuuzwa atapanda watu kichwani, ucsubiri mpaka jina lako, picha yako au mzazi wako idhalilishwe, amkeni, mi ata nikibaki mwenyewe nitasimama kusema ukweli, Mange ni Bully na mnyama anaetugawa ili atuendeshe kwa maslahi yake sio ya nchi".