Msanii wa Muziki wa bongofleva Harmonize anatarajia kuachia remix ya ngoma ya #SingleAgain aliyomshirikisha msanii Ruger kutokea nchini Nigeria siku ya kesho,Ijumaa.
Kupitia instastory yake, Harmonize anasema kuwa Remix ya Single Again ndio Kolabo ya Ruger ya kwanza kuifanya ndani na nje ya Africa.Na msanii huyo anaamini kuwa Remix ya wimbo wake wa Single Again ndio wimbo utakaoshika historia ya kuongoza katika billboard au chati za muziki.
Mbali na hilo Harmonize ameendelea kuonesha mafanikio makubwa ya wimbo wake wa #SingleAgain katika Platform mbalimbali ikiwemo Sportify ikiwa na Streams Milioni 5 na kusema kuwa wimbo huo ndio wimbo wa kwanza Tanzania kufikisha Streams hao ndani ya mwaka huu 2023.
(Imeandaliwa na Happyness John)