Loading...

Rapa Travis Scott akamatwa na Polisi sababu ya makosa mawili

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 weeks ago
rickmedia: rapa-travis-scott-akamatwa-polisi-sababu-makosa-mawili-372-rickmedia

Rapa kutoka nchini Marekani Travis Scott akamatwa na Polisi kisa kulewa hadharani huko Florida huku akiwa na Bunduki.

Rapa huyo alitiwa mbaroni na polisi katika Miami Beach Marina mapema leo Alhamisi asubuhi na kufungwa jela ya kaunti hiyo kwa kosa la unyanyasaji na ulevi.

Sio mara yake ya kwanza kushikiliwa na polisi Travis aliwahi kukabiliwa na kesi ya madai baada ya watu 10 kufariki kufuatia msongamano wa watu wakati wa tamasha lake la 2021 la Astroworld.