Daktari Amuua Mwanamke Mjamzito kisha Kumchukua Mtoto na Kumuuza

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 year ago
rickmedia: daktari-amuua-mwanamke-mjamzito-kisha-kumchukua-mtoto-kumuuza-24-rickmedia

Daktari mmoja aliyekamatwa mwezi Oktoba kwa tuhuma za kusafirisha watoto wanne katika maeneo tofauti nchini Nigeria amekamatwa tena kwa kosa la kumuua Mwanamke mjamzito kwa kumfanyia upasuaji na kisha kuchua mtoto na kwenda kumuuza .

#DkHappinessEnyinnayaIheukeumere, almaarufu #DkHagi, anatuhumiwa kwa k!kumuua mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 20 na kumuuza mtoto wake mchanga.

#DkHagi wa Kituo cha Matibabu cha Hagi, kilichopo barabara ya soko la Abohga Igwuruta, Port Harcourt, anadaiwa kumfanyia upasuaji mjamzito aliyetambulika kwa jina la #RachealSampson ili kumtoa mtoto wake mchanga.

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Dk Happiness alimwambia nesi aifahamishe familia yao kuwa Racheal alifariki kwa ajali ya gari.