Waandishi wa Habari Abdallah Nanda wa kituo cha Channel Ten na Josephine Kibiriti wa Sahara Media Group wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali.
Ajali hiyo iliyohusisha gari dogo imetokea majira ya usiku wa kuamkia leo March 26 eneo la Nyamwage Mkoa wa Kipolisi Rufiji (Pwani)
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea Dar es Saalam kwenye mafunzo kurejea Mkoani Lindi.
"Waliofariki ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Sahara Media group, Josephin Kibiriti na Abdalah Nanda wa Channel Ten na mtu mmoja amejeruhiwa aliyekuwemo ndani ya gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Mziray Abedi, mkazi wa Lindi,"amesema RPC Mutayoba.
Amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Kituo cha afyà Ikwiriri pamoja na majeruhi huyo anaendelea kupata matibabu kwenye kituo hicho