Rais wa Cameroon Apata Pigo Kutoka kwa Binti Yake Brenda Biya Kabla ya Uchaguzi wa 2025

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: rais-cameroon-apata-pigo-kutoka-kwa-binti-yake-brenda-biya-kabla-uchaguzi-283-rickmedia

Rais wa muda mrefu wa Cameroon, Paul Biya, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1982, amekumbwa na pigo kisiasa baada ya binti yake, Brenda Biya — anayejulikana pia kwa jina la kisanii "King Nasty" kutoa wito kwa wananchi kutompigia kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Kupitia ujumbe wake wa wazi kwa wananchi, Brenda aliikosoa vikali serikali ya baba yake, akiituhumu kwa kushindwa kukabiliana na umasikini, ukosefu wa ajira, na mateso ya raia. Aidha, alitoa msamaha kwa niaba ya familia yake kwa mateso na changamoto ambazo wananchi wa Cameroon wamepitia chini ya utawala wa Biya.

Rais Biya, ambaye utawala wake wa zaidi ya miongo minne umeandamwa na shutuma za wizi wa kura na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa, anakabiliwa na ongezeko la upinzani wa ndani, hata kutoka kwa familia yake mwenyewe, hali inayoibua maswali kuhusu mustakabali wa kisiasa wa taifa hilo.