Chad imetangaza nia ya kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ikisema kuwa ufanisi wa mahakama hiyo umekuwa mdogo, na pia ina ubaguzi dhidi ya mataifa ya Afrika.
Taifa hilo limesema kesi tisa kati ya 13 za mahakama hiyo zinahusu nchi za Afrika, na watu sita kati ya saba wanaoshikiliwa wanahusishwa na mambo yaliyotendeka Afrika.