Denmark yasitisha kufunga Ubalozi wake Nchini Tanzania

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 months ago
rickmedia: denmark-yasitisha-kufunga-ubalozi-wake-nchini-tanzania-644-rickmedia

Serikali ya Denmark imebatilisha uamuzi wa kufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024.

Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, uamuzi huo umekuja kufuatia mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika mjini Algiers, Algeria mwezi uliopita ambao ulihusisha nchi tano za Nordic ikiwemo Denmark.

“Mapema leo mwenzangu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark, Lars Løkke Rasmussen, amenifahamisha kuwa serikali ya Denmark inabatilisha uamuzi wake wa kufunga ubalozi wake nchini Tanzania. Kwa hivyo, Denmark itaendelea na historia ya uwepo wake wa miaka 60 nchini Tanzania. Nimepokea habari hii kwa furaha, nikifahamu maana ya uhusiano kati ya nchi zetu mbili,” amesema Makamba.