Kampuni ya poda za watoto kulipa Trilioni 14.5 kumaliza kesi ya poda za watoto

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: kampuni-poda-watoto-kulipa-trilioni-145-kumaliza-kesi-poda-watoto-608-rickmedia

Kampuni ya Johnson & Johnson italipa takribani TZS trilioni 14.5 kusuluhisha kesi nchini Marekani zinazodai kuwa poda ya watoto na bidhaa nyingine zenye madini ya talc zilisababisha saratani ya ovari.

Makubaliano hayo yanahusu takribani madai 76,000, yakiwemo yaliyowasilishwa katika mahakama ya shirikisho na mahakama mbalimbali za majimbo nchini Marekani.