Loading...

Serikali ya Zimbabwe yaipa kibali kampuni ya Elon Musk 'Starlink' kutoa huduma za Intaneti

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 weeks ago
rickmedia: serikali-zimbabwe-yaipa-kibali-kampuni-elon-musk-starlink-kutoa-huduma-intaneti-903-rickmedia

Mamlaka ya Udhibiti wa Posta na Mawasiliano (POTRAZ) imeidhinisha leseni ya utoaji Huduma za Intaneti kwa Kampuni ya Starlink inayomilikiwa na Bilionea Elon Musk

Taarifa ya Rais Emmerson Mnangagwa imesema “Uamuzi huu unatarajiwa kuongeza Miundombinu ya Mtandao wenye Kasi ya Juu na ya gharama nafuu kote nchini nhasa katika maeneo yote ya vijijini.”

Uidhinishaji wa Starlink umekuja baada ya kuwepo msako mkali nchini humo dhidi ya Watumiaji wa huduma hizo ambao hawajasajiliwa na wanaouza vifaa vya Starlink kinyume na Sheria.

Hadi sasa, Starlink imepata Leseni za huduma katika Nchi za Nigeria, Msumbiji, Zambia, Kenya na Malawi. Aidha, hivi karibuni Nchi za Tanzania na Cameroon zilikamata waingizaji wa Vifaa hivyo wasiokuwa na Vibali.