TMA yataja sababu Mvua zinazonyesha kipindi cha Kipupwe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 months ago
rickmedia: tma-yataja-sababu-mvua-zinazonyesha-kipindi-cha-kipupwe-214-rickmedia

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, mvua zinazoendelea kunyesha tangu jana katika baadhi ya mikoa nchini zimetokana na kuongezeka kwa joto la bahari magharimbi mwa Bahari ya Hindi katika mwambao wa pwani wa nchi.

Mvua hizo ziliibua sintofahamu kutokana na majira ya Juni kuwa ya kipupwe, huku TMA ikitaja mikoa ambayo inapata mvua hizo.

Mikoa hiyo ni yote ya ukanda wa Pwani,ukanda wa ziwa Victoria kwenye mikoa ya Kagera, Simiyu, Geita na Mara na maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla leo Jumatano Juni 19, 2024 amesema kwamba mvua hizo hazina madhara.

Amesema, kwenye ukanda wa pwani mvua zitayesha leo Juni 19 na kesho Juni 20 kisha itapungua na vipindi vya jua vitaendelea kama kawaida baada ya siku hizo mbili.

"Hata mikoa mingine, si kama zitakuwa na muendelezo, mifumo inaonyesha ni za kutafuta na ilionekana katika msimu huu wa kipupwe pamoja na kuwa na vipindi vya ukavu na upepo mkali, kutakuwa na mvua kutokana na kuongezeka kwa joto Magharibi mwa Bahari ya Hindi." amesema.